Genesis 5:12-17

12 aKenani alipokuwa ameishi miaka sabini, akamzaa Mahalaleli. 13Baada ya kumzaa Mahalaleli, Kenani aliishi miaka 840, akawa na watoto wengine wa kiume na wa kike. 14Kenani aliishi jumla ya miaka 910, ndipo akafa.

15Mahalaleli alipokuwa ameishi miaka sitini na mitano, akamzaa Yaredi. 16Baada ya kumzaa Yaredi, Mahalaleli aliishi miaka 830, akawa na watoto wengine wa kiume na wa kike. 17Mahalaleli aliishi jumla ya miaka 895, ndipo akafa.

Copyright information for SwhKC